NYOTA WETU
Msanii mkogwe kutoka marekani Lady Luck akiwa katika mahojiano na hip hop dox ameelezea kusikitishwa na ugomvi kati ya Nicki Minaj na Megan Thee Stallion,
Lady Luck amesema kwamba kitendo cha Nicki kumtaja marehemu Mama wa Megan kwenye mzozo ni kuvuka mipaka. Amesema anampenda sana Nicki lakini anahisi mistari hiyo haina heshima, Pia amesisitiza umuhimu wa vita vya rap kuzingatia sanaa badala ya kutoa maneno yenye kuvuruga au kuchafuana.
Lady Luck ameonyesha kutoelewa vita vya rap vimefikaje hapa, akielezea hamu yake ya kuona vita vya rap vinazingatia zaidi ustadi wa kisanii kuliko kutolewa kwa maneno yenye utata. Pia, ameshutumu mbinu za Nicki kwenye ugomvi huo, akimkosoa kwa kulinganisha matukio mabaya, kama shambulio la risasi la Megan na tukio la kushambuliwa la Chris Brown dhidi ya Rihanna.