MAKALA
Kila mwaka tarehe 8 Machi ni Siku ya Kimataifa ya Wanawake ambayo huadhimishwa ili kuheshimu mafanikio ya wanawake, kuongeza uelewa kuhusu tofauti za kijinsia na ubaguzi, na pia kukuza msaada wa kimataifa kwa wanawake.
[Mambo 5 usiyojajua kuhusu International Women Day]
1. Mnamo tarehe 28 Februari 1909, Chama cha Kisoshalisti cha Marekani kilichokuwa hai wakati huo kilisherehekea Siku ya Kitaifa ya Wanawake ya kwanza katika ukumbusho wa wanawake 15,000 walioandamana New York dhidi ya mazingira magumu ya kazi na mishahara midogo.
2. Kwa mwaka 1910, Clara Zetkin ambaye alikuwa mtetezi wa kwanza wa haki za wanawake na kiongozi wa Ofisi ya Wanawake wa Ujerumani kwa Chama cha Kidemokrasia cha Kijamii, alipendekeza wazo la Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani.
3. Tarehe 19 Machi 1911 ilifanyika siku ya kimataifa ya Wanawake na zaidi ya watu milioni 1 katoka Austria, Denmark, Ujerumani na Uswisi walishiriki.
4. Ilichukua hadi 1975 kwa Umoja wa Mataifa kutambua na kuanza kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake (IWD). Ambapo Ttangu wakati huo, Umoja wa Mataifa umekuwa mfadhili mkuu wa tukio hilo la kila mwaka, ukizitia moyo nchi nyingi zaidi kutambua umuhimu wake.
5. Alama ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake ni ishara ya jinsia ya kike na kawaida hufuatana na rangi ya zambarau, kijani na nyeupe, Kulingana na tovuti ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake, rangi ya zambarau inawakilisha utu na haki, kijani kibichi kwa matumaini, na nyeupe kwa usafi. “Rangi hizo zilitoka kwa Umoja wa Kijamii na Kisiasa wa Wanawake (WSPU) nchini Uingereza mnamo 1908.