MICHEZO
Wananchi wameendeleza mwenendo mzuri wa ushindi baada ya kuchukua alama zote tatu mbele ya Wauaji wa Kusini katika dimba la Majaliwa, Ruangwa licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji wake muhimu kama Djigui Diarra, Khalid Aucho, Joyce Lomalisa, Pacome Zouzoua na Kennedy Musonda.
FT: Namungo Fc 1-3 Yanga Sc Bacca (og) 69′
Mudathir 54′
Mzize 58′
Aziz Ki 63′
Yanga Sc imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu bara ikifikisha alama 46 baada ya mechi 17 ikiwa alama mbili mbele ya Waoka Mikate, Azam FC waliopo nafasi ya pili. Azam Fc imecheza mechi tatu zaidi ya Yanga Sc.
Namungo Fc inasalia nafasi ya 7 alama 23 baada ya mechi 20.

Related Content
Related Content
Related News 
Watuhumiwa wanne kati ya sita wanaokabiliwa na kesi ya kubaka...
Bundesliga leaders Bayern Munich scored three times in 19 minutes...
Kenya's Ruth Chepngetich put on a performance for the ages...