NYOTA WETU
Bondia Francia Ngannou raia wa Cameroon amewaomba radhi mashabiki wake kwa kuwaangusha kufuatia kichapo cha ‘Knock Out’ kwenye raundi ya pili kutoka kwa Anthony Joshua.
Anthony Joshua alishinda pambano lake la nne mfululizo kwa kupata ushindi kwa ‘Knock Out’ kwenye raundi ya pili dhidi ya bondia Ngannou mjini Riyadh, Saudi Arabia.
Ngannou aliwashangaza mashabiki alipomcharaza Fury kwenye pambano la mwaka jana hali iliyopelekea mashabiki kuamini angeweza kumshangaza Joshua.
Hata hivyo Joshua aliwanyamazisha waliokuwa na shaka, akimtoa Ngannou katika raundi zote mbili na akatoa kauli kama alivyoahidi ya ushindi wa KO ndani ya dakika tano tu za pambano lao.
Licha ya kichapo hicho Ngannou alitia kibindoni kitita cha Dola milioni 20 huku Joshua alipokea Dola Milioni 50.