JOHN CENA APANDA JUKWAANI AKIWA UCHI

0:00

NYOTA WETU

Mwanamieleka wa zamami ambaye kwa sasa Muigizaji John Cena amewashangaza wengi baada ya kupanda kwenye Jukwaa la tuzo Oscars 2024 jana Machi 10, 2024 na kutangaza washiriki wa kipengele cha vazi bora la ubunifu katika filamu akioneka hajavaa chochote zaidi ya kujifunika na bahasha sehemu zake za siri.

Nyota huyo alipanda jukwaani kwa kusitasita ikiwa ni mpango wa kuigiza tukio kama hilo lililowahi kutokea katika tuzo za 46 za Oscars mwaka wa 1974 wakati David Niven alipokuwa akimtambulisha Elizabeth Taylor akiwa katika hali ya nusu utupu.

John Cena aliwasilisha tuzo hiyo ya ubunifu wa mavazi bora zaidi katika Tuzo za Oscar za 2024 bila chochote isipokuwa [kibao] hicho kilichokuwa kimemfunika kidogo akiwa na bahasha kubwa iliyoshikiliwa kwenye mapaja yake, Japokuwa nyota huyo wa “Fast X” alionekana akiwa uchi kabisa alipopanda jukwaani, picha za nyuma ya jukwaa zinafichua kuwa alikuwa amevalia vazi la kujikinga ambalo lilifunika sehemu zake za siri tu.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Mfahamu Rais Mpya wa Iran Masoud Pezeshkian
Don't miss out!
Invalid email address