WATU 9 WAFARIKI BAADA YA GARI LAO KUSOMBWA NA MAJI

0

0:00

HABARI KUU

Watu tisa wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noah lenye namba za usajiri T795 BIS kusombwa na maji kwenye mto Kisimani katika Kijiji cha Lumeme kilichopo Halmashauri ya Nyasa Mkoani Ruvuma.

Akithibitisha kutokea kwa tulio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya amesema tukio hilo limetokea Machi 11, 2024 baada ya gari hilo kusombwa na maji.

Amesema, chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva ambaye alilazimisha kuvuka wakati Mto huo ukiwa umejaa maji, na kutoa rai kwa Madereva na Wananchi kuacha tabia ya kupima maji katika madaraja kwa kuyatazama.

Amewataja waliofariki kuwa ni Edwini Abeli Ngowoko (55), Matengo (Dereva wa Gari), Valeliana Ndunguru (18), Innocent Cassian Ndunguru ( 63), Simon Mahai (21) na Nathan Kumburu (39).ā€

ā€œWengine ni Faraja Daud Tegete (18) ambaye ni Mwanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari Kilumba, Ebiati Daud Tegete (2) na Alfonsia Casian Mbele (40).

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  ERIKA DE SOUZA VIEIRA APELEKA MAITI BENKI KUKOPA PESA
Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading