0:00
MAPENZI
Nani alikwambia wewe ni mtu mzima hata kama una miaka zaidi ya 40 upo tayari kuingia kwenye ndoa? Hizi ndizo dalili za mtu ambaye hayuko tayari kuoa / kuolewa.
- Hauna maono kuhusu maisha yako. Hujui unachotaka,jinsi ya kukipata na jinsi ya kuvutia mtu sahihi wa kukusaidia kutimiza maono yako
- Hauna hata chanzo kimoja cha kipato. Unapewa tu chakula na kupewa mahitaji mengine.
- .Hauna kazi,huna ndoto,huna matamanio, huna maono. Ni mtu upo upo tu.
- Wewe ni mtu wa hisia kali/hasira.
- Wewe ni mwepesi wa wivu,usiyethamini au kujithamini.
- Wewe ni mtu usiye na kiasi. Unaendeshwa na hisia. Unaongea bila mipaka,unatembea bila mipaka. Unalala tu ukiamua,unafanya chochote bila kuwaza au kutafakari.
- Wewe ni mtu usiyetii Mamlaka.
- Huna mahusiano na MUNGU. Huna muda wa kuhudhuria ibada au kusoma vitabu vya dini.
- Huwezi kupika hata chakula na hata kufanya usafi wa nyumba.
- Wewe ni mvivu,mtu wa kulala tu,unafanya mambo taratibu na mambo kama haya.
- Unachukia Tendo la ndoa
- Ni muoga wa tendo la ndoa
- Ni mwanaume au Mwanamke mzinifu
- Ni Mbaguzi sana ,yaani kuna watu (wanawake/wanaume) hawakufai
- Unapenda kusema uongo.
- Unapenda kutamba. Husemi ni kipi unapenda na jinsi unavyojisikia.
- Wewe ni mtu usiyethubutu
- Wewe ni mkatili,mwenye kujipendelea,unayejiona mwenyewe, kiburi,usiye na busara,unayejitenga,mkorofi na mkali.
- Hupendi watoto.
- Unafuja na kupoteza pesa au huoni thamani ya pesa.
- Unapenda kuwa chini (hasa Mwanaume).
- Ni mwepesi au dhaifu.
- Huna muda kujifunza kuhusu ndoa hata kama unaona vitabu au machapisho.
- Una wapenzi wengi.
- Unachukia waliopo kwenye Ndoa.
- Ni mbinafsi
- Ukiwa Mtenda dhambi.
Related Posts 📫
-Female Psychology Thread-
Reason 1: Penetration Isn’t Everything
Let’s start with the...
HABARI KUU.
Mamlaka inayohusika na mambo ya Afya ya nchini...
MAGAZETI
Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
LOVE TIPS ❤
1. Don't expect your partner/spouse to know...
NYOTA WETU.
Baba Mzazi wa nyota wa Liverpool Luis Diaz...