KAMATI YA BUNGE YALIDHISHWA NA UFUFUAJI WA KMTC

0:00

HABARI KUU

Kamati ya Kudumu ya Bunge, Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Deudatus Mwanyika leo tarehe 14 Machi, 2024 Imepokea na Kujadili Taarifa ya Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), inayohusu Utekelezaji wa Bajeti ya Maendeleo ya Kiwanda cha Kutengeneza Mashine na Vipuri (KMTC) kwa mwaka wa Fedha 2023/2024.

Kiwanda cha KMTC kilichopo katika Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, kimejikita katika uzalishaji wa mashine mbalimbali zikiwemo mashine za kukata na kuchonga, kufua chuma, kuranda mbao, pampu pamoja na vipuri. Lengo kuu la Kiwanda hiki cha KMTC ni kuwa mzalishaji wa mashine za viwandani ili kujenga na kukuza viwanda nchini. Kiwanda hiki kina maeneo makuu ya uzalishaji ambayo ni eneo la karakana ambapo shughuli kuu inayofanywa katika eneo hili ni uchongaji wa vipuri mbalimbali pamoja na kuunda mashine.

Aidha, kiwanda hiki cha KMTC kina vitengo mbalimbali vya uzalishaji ambapo kitengo cha Uundaji kazi yake ni kuunda maumbo na kuunganisha ili kupata mashine. Kitengo kingine ni cha uyeyushaji wa chuma na utengenezaji wa maumbo mbalimbali pamoja na kitengo cha uwekaji utando kwenye chuma ili kisipate kutu.

Hata hivyo, Mhe. Mwenyekiti pamoja na Waheshimiwa wajumbe walimpongeza sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi anavyoendelea kufufua viwanda hususani kiwanda cha KMTC ambacho kilikuwa hakifanyi kazi kwa takriban miaka 29, pamoja na kutoa fedha za maendeleo katika kiwanda hicho. Mwenyekiti aliendelea kumshukuru Waziri wa Viwanda na Biashara kwa kusimamia vyema Uongozi pamoja na wafanyakazi wa kiwanda cha KMTC na kusisitiza kutafuta mali ghafi kwa wingi ili kuendelea kuzalisha vifaa hivyo na si kusubiri mteja mmoja mmoja.

See also  HAWA NDIO WASHINDI WA KUHIFADHI QURAN TUKUFU MWAKA 2024

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Sabalenka to end year as number one...
Coco Gauff beat defending champion Iga Swiatek 6-3 6-4 at...
Read more
Neymar return overshadowed as Al-Dawsari's hat-trick seals...
HONG KONG, 🇭🇰 - Saudi Arabia's Al-Hilal handed defending champions...
Read more
MPANGO YUKO FITI KALIKITI ...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
ONYO KWA WATUMIAJI WA NGUVU ZA KIUME...
MAGAZETI Karibu Mtanzania kwenye magazeti ya leo kwenye mbao za...
Read more
Differences between Broilers and Layer Farming
Broilers and layers are two types of chickens that are...
Read more

Leave a Reply