Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe na Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar.

0:00

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe huku aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya akihamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Martin Otieno aliyehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

Uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Polisi katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

13 WAYS ON HOW TO SETTLE DISAGREEMENTS...
LOVE ❤ 1. Pray for calmness and unity in your...
Read more
Luton condemn racist abuse against striker Adebayo
Luton Town said the club was angry and frustrated after...
Read more
SABABU ZA MBAPPE KULAZIMISHA KUONDOKA PSG ...
MICHEZO Mshambuliaji wa Ufaransa, Kylian Mbappe ameiambia timu yake ya...
Read more
ALICHOFANYA CHAMA MPAKA KUFUNGIWA NA SIMBA ...
NYOTA WETU Klabu ya Simba imewasimamisha, Clatous Chama na Nassor...
Read more
MAGAZETI YA LEO 27 MEI 2024
Read more
See also  HOW TO START AN ONLINE BUSINESS

Leave a Reply