Mkuu wa Wilaya Morogoro Rebeca Nsemwa ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu Diwani Kata Mwembesongo Mhe.Ally Rashidi Kalungwana Kwa kitendo cha Kutumia vibaya madaraka yake kujenga vibanda vya biashara katika eneo la wazi Soko Kuu la chifu Kingalu Manispaa ya Morogoro

0:00

DC Rebbeca amesema Diwani huyo amejenga vibanda vya kufanyia biashara katika Soko Kuu la Chifu Kingalu bila kufuata taratibu za mipango miji jambo ambalo ni kosa kisheria na kutaka achukuliwe hatua za kinidhamu haraka sana Ili iwe fundisho kwa watu wengine.

DC Rebbeca anasema licha ya Diwani huyo kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya mipango miji Halmashauri Manispaa ya Morogoro, lakini amekua mtu wa kwanza kuvunja sheria hivyo lazima awe mfano kwa watu wanaotumia madaraka yao vibaya.

Mwenyekiti wa soko Hilo la Chifu Kingalu, Khalid Mkunyegele anasema licha ya uongozi wa soko kumkataza kujenga lakini alikaidi amri hiyo na kuendelea hadi kamati ya usalama Wilaya ilipofika na kubomoa vibanda hivyo ambayo vimejengwa pembeni ya soko kuu .


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Mikel Arteta says Arsenal's players have told him they "want more" this season as they look to deny Manchester City a fifth consecutive Premier League title.
Don't miss out!
Invalid email address

By Mujuni Henry

JUNIITV

Please disable your adblocker or whitelist this site!

         banner                            

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading