Mkuu wa Wilaya Morogoro Rebeca Nsemwa ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu Diwani Kata Mwembesongo Mhe.Ally Rashidi Kalungwana Kwa kitendo cha Kutumia vibaya madaraka yake kujenga vibanda vya biashara katika eneo la wazi Soko Kuu la chifu Kingalu Manispaa ya Morogoro

0:00

DC Rebbeca amesema Diwani huyo amejenga vibanda vya kufanyia biashara katika Soko Kuu la Chifu Kingalu bila kufuata taratibu za mipango miji jambo ambalo ni kosa kisheria na kutaka achukuliwe hatua za kinidhamu haraka sana Ili iwe fundisho kwa watu wengine.

DC Rebbeca anasema licha ya Diwani huyo kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya mipango miji Halmashauri Manispaa ya Morogoro, lakini amekua mtu wa kwanza kuvunja sheria hivyo lazima awe mfano kwa watu wanaotumia madaraka yao vibaya.

Mwenyekiti wa soko Hilo la Chifu Kingalu, Khalid Mkunyegele anasema licha ya uongozi wa soko kumkataza kujenga lakini alikaidi amri hiyo na kuendelea hadi kamati ya usalama Wilaya ilipofika na kubomoa vibanda hivyo ambayo vimejengwa pembeni ya soko kuu .

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Stalemate at National Consultative Council Meeting in...
A stalemate has erupted at the National Consultative Council (NCC)...
Read more
BURUNDI NA TANZANIA KUFANYA BIASHARA YA PAMOJA
HABARI KUU SERIKALI kupitia Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) imetia...
Read more
HOW TO BE A ROMANTIC WIFE
LOVE TIPS ❤ Remember that romance is not the husband's...
Read more
SVEN BOTMAN APATA MAJERAHA YA GOTI
MICHEZO Beki wa Newcastle United, Sven Botman anatarajia kukaa nje...
Read more
Why children should sleep in their own...
When it comes to bedtime, the sleeping arrangement can significantly...
Read more
See also  TUNDU LISSU Atangaza Nia ya Kugombea Urais wa Tanzania

Leave a Reply