Mkuu wa Wilaya Morogoro Rebeca Nsemwa ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu Diwani Kata Mwembesongo Mhe.Ally Rashidi Kalungwana Kwa kitendo cha Kutumia vibaya madaraka yake kujenga vibanda vya biashara katika eneo la wazi Soko Kuu la chifu Kingalu Manispaa ya Morogoro

0:00

DC Rebbeca amesema Diwani huyo amejenga vibanda vya kufanyia biashara katika Soko Kuu la Chifu Kingalu bila kufuata taratibu za mipango miji jambo ambalo ni kosa kisheria na kutaka achukuliwe hatua za kinidhamu haraka sana Ili iwe fundisho kwa watu wengine.

DC Rebbeca anasema licha ya Diwani huyo kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya mipango miji Halmashauri Manispaa ya Morogoro, lakini amekua mtu wa kwanza kuvunja sheria hivyo lazima awe mfano kwa watu wanaotumia madaraka yao vibaya.

Mwenyekiti wa soko Hilo la Chifu Kingalu, Khalid Mkunyegele anasema licha ya uongozi wa soko kumkataza kujenga lakini alikaidi amri hiyo na kuendelea hadi kamati ya usalama Wilaya ilipofika na kubomoa vibanda hivyo ambayo vimejengwa pembeni ya soko kuu .

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

AJALI ILIVYOUWA WATU 7 MOROGORO
HABARI KUU Watu saba wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa...
Read more
SIGNS THAT YOU ARE TAKING YOUR PARTNER...
YOU DON'T APOLOGIZEIf you care about your partner, it will...
Read more
Social media personality Saida Boj has been...
Okoye’s actions escalated the situation when he impulsively turned to...
Read more
Actress Wofai Fada disclosed her age in...
CELEBRITIES Today, May 11th, 2024, Wofai Fada, a talented actress...
Read more
TB Joshua na sakata la kuwanyanyasa wanawake...
HABARI KUU BBC World Service wamegundundua madudu ya nabii Joshua....
Read more
See also  Gayton McKenzie jambazi sugu aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Michezo

Leave a Reply