Mkuu wa Wilaya Morogoro Rebeca Nsemwa ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu Diwani Kata Mwembesongo Mhe.Ally Rashidi Kalungwana Kwa kitendo cha Kutumia vibaya madaraka yake kujenga vibanda vya biashara katika eneo la wazi Soko Kuu la chifu Kingalu Manispaa ya Morogoro

0:00

DC Rebbeca amesema Diwani huyo amejenga vibanda vya kufanyia biashara katika Soko Kuu la Chifu Kingalu bila kufuata taratibu za mipango miji jambo ambalo ni kosa kisheria na kutaka achukuliwe hatua za kinidhamu haraka sana Ili iwe fundisho kwa watu wengine.

DC Rebbeca anasema licha ya Diwani huyo kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya mipango miji Halmashauri Manispaa ya Morogoro, lakini amekua mtu wa kwanza kuvunja sheria hivyo lazima awe mfano kwa watu wanaotumia madaraka yao vibaya.

Mwenyekiti wa soko Hilo la Chifu Kingalu, Khalid Mkunyegele anasema licha ya uongozi wa soko kumkataza kujenga lakini alikaidi amri hiyo na kuendelea hadi kamati ya usalama Wilaya ilipofika na kubomoa vibanda hivyo ambayo vimejengwa pembeni ya soko kuu .

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

SABABU ZA MAMELODI SUNDOWNS KUWA TISHIO KWENYE...
MICHEZO Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ndiyo wapinzani wa Yanga...
Read more
MAPOROMOKO YA MATOPE YAUA 47 KATESH ...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
MFAHAMU MSANII AYRA STARR WA NIGERIA
MICHEZO/BURUDANI Staa mwimbaji wa muziki wa Afrobeat kutoka Nigeria Ayra Starr...
Read more
Embakasi South MP Calls for Restraint as...
Embakasi South Member of Parliament Musili Mawathe has urged police...
Read more
12 KEYS TO A LASTING MARRIAGE
LOVE TIPS ❤ There is no accidental success or satisfaction...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  LUHAGA MPINA kuwaburuza Spika na Bashe Mahakamani

Leave a Reply