SABABU ZA MGOMO WA MADAKTARI KENYA

0:00

HABARI KUU

Mgomo wa madaktari katika Hospitali za Umma kote Nchini Kenya, umeanza rasmi hii leo Machi 14, 2024, huku baadhi ya jamaa wakilazimika kuwaondoa wagonjwa wao katika Hospitali hizo, ili kutafuta huduma za matibabu kwingine.

Hata hivyo, shughuli za kawaida katika Hospitali kuu ya Rufaa na Mafunzo ya Kilifi zimeendelea, hivyo kukinzana na tamko la Muungano wa Madaktari ukanda wa Pwani – KMPDU, la mgomo wa Madaktari.

Mmoja wa wauguzi aliyeongea kwa sharti la kutotaja jina, amesema wanaendelea na kazi ya kuhudumia wagonjwa kama kawaida, baada ya uongozi wa madaktari Kilifi kufanya mkutano na Serikali ya Kaunti ya Kilifi.

Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno nchini Kenya – KPMDU, ulitangaza mgomo wakiishinikiza Serikali kutimiza mahitaji yao muhimu, ikiwemo kurejeshwa kwa makato ya ushuru wa Nyumba yaliyofanyika katika mishahara yao, ambayo Mahakama ilitangaza kuwa yanafanyika kinyume na Katiba.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Napoli's Conte preparing for emotional clash with...
Napoli manager Antonio Conte acknowledges that Saturday's home game with...
Read more
KOSA LA JK HILI KWA LOWASSA ...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
Musician Davido expresses joy as his uncle,...
Famous Nigerian Afrobeat musician David Adeleke, whose stage name is...
Read more
ORODHA YA WACHEZAJI WALIOTOKA ULAYA NA KWENDA...
Makala Fupi Wachezaji kutoka kwenye ligi za ushindani walioamia kwenye...
Read more
PAUL POGBA ASIKITISHWA NA UAMUZI WA KUMFUNGIA...
MICHEZO Saa kadhaa baada ya kutoka kwa taarifa za Paul...
Read more
See also  MUHIMBILI-MLOGANZILA YAINGIZA BILIONI 8 KISA UREMBO

Leave a Reply