Fenway Sports Group inayoimiliki klabu ya Liverpool imetangaza kumrejesha Edwards kama Mkurugenzi Mtendaji mpya wa klabu hiyo.
Edwards alipata mafanikio makubwa akiwa na Liverpool kwenye historia ya klabu hiyo, akifanya kazi sambamba na Klopp kutengeneza kikosi kilichoshinda ubingwa wa Ligi Kuu ya England na Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.
Kiongozi huyo aliondoka Liverpool mwaka 2022, lakini pamoja na kukataa nafasi ya kurejea kwenye klabu hiyo mapema mwaka huu, sasa amefikia makubaliano ya kuwatumikia tena wekundu hao wa Anfield.
Taarifa ziliibuka kwamba moja ya mazungumzo yake ya kwanza baada ya kurejea kwenye klabu hiyo ilikuwa kumshawishi Klopp kubaki kitu ambacho kocha huyo amekikanusha.
Klopp alipoulizwa kama habari hizo ni za kweli, alisema: “Hapana. Haikuwa mada tuliyozungumza. Unaweza kufikiria kama nikibadili uamuzi sasa. Sikuwa nimefanya maamuzi yangu kwa kufikiria.”