Korea Kaskazini imepiga marufuku wananchi wake kufuga mbwa na kuishi nao kama sehemu ya familia, badala yake imetakiwa kufuga kwa ajili ya kula nyama na kuchuna ngozi yake kwa matumizi ya viwandani.
Chanzo kimoja kikizungumza na Daily NK kiliorodhesha makosa ambayo mmiliki wa mbwa anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria, Ambapo makosa hayo ni ufugaji mbwa kama mwanafamilia.
“Kumfanya mbwa kama sehemu ya familia, kula na kulala naye kwenye familia ni kinyume na maelekezo ya serikali na kinatakiwa kuepukwa na haiendani na mtindo wa maisha wa ujamaa kabisa.” alisema mtoa taarifa.
Makosa mengine yaliyoorodheswa ni pamoja na kumvalisha mbwa nguo kama ambavyo baadhi ya watu mashuhuri duniani wamekuwa wakifanya kwa mbwa wao.
Hatua hii ya kiongozi Kim Jong Un Rais wa nchini humo inaonekana kulenga kuusaidia umma kwenye hali mbaya ya kiuchumi pamoja na uhaba wa chakula nchini humo.