Wakati watu wengi nje ya Liverpool wakimuona kama ni mbinafsi na anajiangalia yeye tu, mshambuliaji wa timu hiyo Mohamed Salah amewaziba mdomo waliodhania tofauti.

0:00

Salah amekuwa na mchango mkubwa kwa Liverpool tangu ajiunge nayo mwaka 2017 akiisaidia kushinda Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa, Carabao na FA Cup.

Msimu huu Liverpool inashiriki michuano ya Europa ikiwa ni baada ya kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa msimu uliopita na mara nyingi kwenye michuano hii wameonekana kutumia wachezaji vijana kutoka kwenye akademni yao.

Inaelezwa kwamba Salah ndio amekuwa akiwasimamia wachezaji hao na kuongea nao mara tu wanapokuwa wanapandishwa kwenye kikosi cha kwanza tofauti na ilivyodhaniwa kwamba, jamaa anaringa na hapendi wenzake wafanikiwe.

“Kitu kikubwa ambacho nakifanya ni kuzungumza nao, na kuonyesha kwamba unawajali kabla hata ya kuwapa ushauri wowote, kama ukiwapa tu ushauri bila ya kuwaonyesha kama unawajali wanaweza wasisikilize ushauri wako.

“Lakini kama utamuonyesha kumjali na kumwambia kwamba ataenda kufanya mambo makubwa na ataonyesha kiwango bora na akienda uwanjani afanye tu vitu vidogo ili kubadilika siku hadi siku, mimi kila siku nawaonvesha kwamba nawajali kisha baada ya hapo inakuwa rahisi kuongea nao na kuwaweka mkononi.”

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Nottingham Forest midfielder Danilo has suffered a...
The 23-year-old fell badly on his left leg when challenging...
Read more
Anita Joseph rants about an experience with...
Nollywood actress Anita Joseph recently took to social media to...
Read more
HOW WOMEN CAN EXPERIENCE ORGASM EASILY
LOVE TIPS ❤ We learnt that orgasm is the most...
Read more
Portugal close in on Nations League quarters...
GLASGOW, Scotland, 🏴󠁧󠁢󠁳󠁣󠁴󠁿 - Portugal all but sealed a berth...
Read more
Former Somali Minister Endorses Raila Odinga for...
Former Somali Foreign Affairs Minister Fawzia Yusuf Adam has thrown...
Read more
See also  MOHAMED SALAH AWAGOMBANISHA LIVERPOOL NA EFA

Leave a Reply