HABARI KUU
Serikali ya Burundi imesema Mfanyabiashara atakayekamatwa akiwa anapeleka biashara nchini Rwanda ataadhibiwa kama adui wa nchi.
Hayo yamesema na Mkuu wa Mkoa wa Cibitoke, Careme Bizoza wakati akizungumza na Wakuu wa Wilaya, Madiwani na Wenyeviti wa Mkoa huo unaopakana na Rwanda.
Wananchi wa mkoa huo wamesema kuwa hatua hiyo ni kama kuwafunga mikono nyuma kwani ndipo walipokuwa wanatoa fedha kwa ajili ya kuziendesha familia zao.
Wameutaka uongozi wa Burundi kuifungua mipaka dhidi ya Rwanda iliyofungwa mwanzoni mwa mwaka huu.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.