DE BRUYNE NA MANCHESTER CITY BADO NGOMA NZITO

0:00

MICHEZO

Mabosi wa Manchester City wamesitisha mazungumzo na wawakilishi wa kiungo Kevin de Bruyne yaliyokuwa na lengo la kumsainisha mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Mazungumzo hayo yamesitishwa kwa kile kinachoelezwa wanaweka umakini zaidi kwenye mechi za timu hiyo katika michuano mbalimbali.

De Bruyne mwenye umri wa miaka 32, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2025, na hivi karibuni Man City ilidaiwa kuwa tayari kumuuza ikipata ofa nono.

Mara kadhaa matajiri kutoka Saudi Arabia wameonyesha nia ya kumsajili nyota huyu na kuwa tayari kutoa zaidi ya Pauni 100 milioni kama ada ya uhamisho na kumpa mshahara mara tatu ya ule anaoupokea Man City kwa sasa.

Hata hivyo, baada ya kusambaa kwa taarifa hizo, Man City iliingia naye mazungumzo ili asaini mkataba wa kuendelea kuitumikia kwani kocha Pep Guardiola bado anahitaji huduma yake.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

BURUNDI NA CONGO ZAUNGANA KUIPIGA RWANDA
HABARI KUU. Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye amesema atawasaidia vijana...
Read more
Terrorists behind Borno bomb attack will pay...
President Bola Tinubu has vowed that the terrorists behind the...
Read more
Impeached Deputy President Rigathi Gachagua Discharged from...
Impeached Deputy President Rigathi Gachagua recounted the alarming moments leading...
Read more
Siri yafichuka AZIZ KI kumvuta nyota huyu...
TETESI Staa wa Yanga Aziz Ki ni swahiba mkubwa wa Chama....
Read more
ISRAEL YAISHAMBULIA GAZA USIKU KUCHA ...
MAGAZETI Karibu Mtanzania kwenye magazeti ya leo kwenye mbao za...
Read more

Leave a Reply