Kama ulikua hujui kuwa duniani kuna sehemu bahari ya PASIFIKI na ATLANTIC zinakutana lakini maji yake HAYA CHANGANYIKI wacha nikufahamishe;-
Unachokiona hapo sio uongo ni ukweli mtupu,
Hizo ni BAHARI MBILI zinakutana hapo ambazo ni PASIFIC na ATLANTIC,
Bahahari mbili za ATLANTIC na PACIFIC kuna sehemu zinakutana,
Lakini cha ajabu maji hayo yanaonekana kutochanganyika,
Upo mpaka kabisa katika maji unao yatofautisha maji ya bahari moja na bahari nyingine,
Upande mmoja yakionesha kuwa na rangi tofauti na ya upande wa pili,
Wengine wanalihusisha tukio hili na nguvu za giza,
Wengine wanaeleza ni miongoni mwa ishara kwamba,
Mungu yupo na wengine hawaelewi chochote.

SABABU YA KUWA HIVI NI NINI?

Kuweka mambo sawa lazima ieleweke kwamba,
Si kwamba maji ya bahari hizo mbili hayachanganyikani si kweli,
Isipokuwa huchukua muda kidogo kuchanganyikana,
Na hii hutokea kwa sababu
PACIFIC ndiyo bahari kubwa kuliko zote duniani,
Ikikusanya maji kutoka ANTARCTICA mpaka ARCTIC,
Yaani kuanzia ncha ya KASKAZINI mpaka ncha ya KUSINI ya dunia,
Kwa kuwa sehemu kubwa ya vyanzo vya maji yake ni theluji,
Hivyo kiwango cha chumvi kwenye maji ya bahari hiyo,
Ni kidogo ukilinganisha na maji ya bahari ya ATLANTIC,
Na hii theluji imetokana na baridi kali iliopo kwenye ncha ya Dunia,
Kisayansi maji yenye kiwango tofauti cha chumvi,
Huchukua muda mrefu sana kuchanganyikana,
Na ushahidi wa hili ni kwamfano eneo ambalo mto AMAZON unaingiza maji baharini,
Kwa kuwa maji ya mto hayana chumvi tofauti na ya baharini,
Ukiwa umbali wa zaidi ya mita 200 baharini,
Kutoka usawa wa eneo hilo kuna maji baridi yasiyo na chumvi kabisa.

SABABU ZA KITAALAMU YA MAJI HAYO KUWA HIVYO NI KAMA ZIFUATAZO;-

1) Utofauti wa kiwango cha chumvi kati ya bahari hizo mbili,
Bahari ya ATLANTIC ndio bahari yenye chumvi nyingi zaidi kuliko bahari zote duniani.

2) Maji ya Bahari ya ATLANTIC yanajongea kuelekea upande wa Kusini,
Wakati huohuo maji ya PACIFIC yenyewe,
Yanajongea kwa mfumo ambao kitaalamu huitwa circumpolar movement,
Yaani mwendo wa kuzunguka kutoka ncha moja ya dunia mpaka nyingine,
Kwa lugha nyepesi ni kwamba maji ya Bahari ya PACIFIC,
Yanajongea kwa mfumo wa kuzunguka duara lakini yakitokea Mashariki,
Mkondo wa Bahari ya ATLANTIC una nguvu zaidi kwa sababu una uelekeo mmoja,
kwa hiyo katika eneo maji yanapo kutana,
Maji ya ATLANTIC yanakuwa kwenye kasi tofauti inayokinzana na maji ya PACIFIC,
Kwa hiyo yanalazimika kusafiri kwenye mstari mmoja ulionyooka,
Kwa umbali fulani kabla ya baadaye kuanza kuchanganyikana.

3)Kasi ya maji ya juu ya bahari, ni tofauti na kasi ya maji ya chini ya bahari,
Kwa hiyo pale bahari hizo mbili zinapokutana,
Maji yanayoanza kuchanganyikana huwa ni ya chini kwa sababu ya kasi yake kisha baadaye,
Ndiyo maji ya juu nayo huchanginyakana taratibu kwa sababu ya kasi yake.

Hayo maji ya blue ni maji ya bahari ya PASIFIC,
Na hayo maji meupe ndio maji ya bahari ya ATLANTIC.

0:00

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Pep Guardiola has made it clear he...
The striker has starred for City since arriving in the...
Read more
MBARONI KWA KUMNYONGA MKEWE
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
Six (6) darkest manipulation Tactics women used...
Let's get started 1). Emotional Blackmail: Emotional Blackmail is one of...
Read more
Norris defies orders to help Piastri and...
LUSAIL, Qatar 🇶🇦 — Lando Norris ignored team orders and...
Read more
HOW TO KNOW IF THE LOVE IS...
When someone loves you, you know and you will feel...
Read more
See also  Kwanini Kauli ya Nape Nnauye Imepigwa na Wanaharakati?

Leave a Reply