MICHEZO
Kevin De Bruyne ameachwa nje ya kikosi cha Ubelgiji kwa ajili ya mechi za kimataifa baada ya kupata majeraha ya nyonga.
Akiwa amekosa miezi minne ya kampeni kutokana na jeraha la msuli wa paja, De Bruyne amekuwa katika hali nzuri tangu arejee Januari na sasa ana asisti 13 katika mechi 14 za mashindano yote pale Manchester City. Asisti yake ya hivi karibuni ilikuja katika sare ya 1-1 dhidi ya Liverpool.
Na sasa Kocha wa Ubelgiji, Domenico Tedesco, amefichua De Bruyne hayuko sawa kabisa na ameachwa nje ya kikosi cha Ubelgiji kutokana na hilo.
De Bruyne hataonekana katika mechi ya Robo Fainali ya Kombe la FA baadae leo Jumamosi (Machi 16) dhidi ya Newcastle United kutokana na tatizo hilo.
Baada ya mapumziko ya kimataifa, City watarejea uwanjani wakiwa na mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya wapinzani wao Arsenal kwenye Uwanja wa Etihad.
Guardiola atamtaka De Bruyne awe fiti kwa ajili ya mchezo huo, na hivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 ambaye ataachwa nyumbani wakati wa mapumziko ya kimataifa atakuwa msaada mkubwa kwa bosi wa City.