Katika hotuba ya Dkt. Kikwete wakati wa hafla hiyo iliyoandaliwa na Jarida la Uongozi Afrika (ALM) jijini Addis Ababa, Ethiopia ameshukuru kwa kutunukiwa tuzo hiyo na kuwasihi Waafrika wote kwenye nafasi za uongozi kutoa kipaumbele kwenye masuala kutatua changamoto zilizopo ikiwemo umasikini, changamoto ya chakula, mabadiliko ya tabia ya nchi, magonjwa, ujinga, migogoro ya kisiasa na vita.
“Ukweli ni kwamba, ni kwa heshima kubwa ninakubali kupokea tuzo hii. Naipokea,
si tu kwa ajili yangu bali kwa niaba ya Waafrika wengine wengi; wawe viongozi wa kisiasa, wenye ushawishi kiuchumi, viongozi wa dini, wanachama wa vikosi vya usalama, watumishi wa umma, na wananchi wa kawaida ambao huamka kila siku na kufanya sehemu yao katika kulifanya Bara la Afrika kuwa sehemu nzuri zaidi ya kuishi,” amesema Dkt. Kikwete.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.