JENERALI VENANCE MABEYO ASIMULIA MAGUFULI ALICHOMWAMBIA KABLA YA UMAUTI

0:00

NYOTA WETU

Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Venance Mabeyo amesema siku moja kabla ya kifo cha Hayati John J. Magufuli, alimwita na kumwambia anajua hawezi kupona na hivyo awaagize Madaktari wamrudishe nyumbani kwake.

Mabeyo amesema “Aliniita CDF njoo, siwezi kupona, waamuru hawa Madaktari wanirudishe nyumbani. Nikamjibu Mheshimiwa sina Mamlaka hayo, suala la Afya sio la CDF, naomba ubaki Madaktari watatuambia”

Katika Makala aliyofanya na Waandishi wa Habari kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), ameongeza kuwa Machi 17, 2021 saa 8 mchana, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama waliambiwa hali ya Rais Magufuli imebadilika na ilipofika saa 12:30 Jioni alifariki.”Siku moja kabla ya kifo chake hali ilibadilika kidogo na yeye alijitambua kwamba hali imebadilika, na nadhani alijua Mwenyezi Mungu alimuongoza kwamba hatapona alichosema nirudisheni nyumbani nikafie nyumbani nikasema mheshimiwa hapana hapa upo kwenye mikono salama madaktari wapo waendelee kukutibu”

“Niseme jambo moja ambalo halikuwahi kusemwa huko nyuma kwa sababu nilikuwepo pale aliniita CDF (Mkuu wa Majeshi) njoo akaniambia siwezi kupona ,waamuru hawa madaktari wanirudishe nyumbani nikamwambia mheshimiwa sina mamlaka hayo, akasema yaani CDF unashindwa kuwaamuru madaktari wanirudishe nyumbani, nikamwambia suala la afya siyo la CDF mheshimiwa naomba ubaki utulie madaktari watatuambia”

“Alipoona kwamba nimekuwa na msimamo huo akaniambia niitieni paroko wangu, Paroko wa St.Peters Father Makubi lakini akaongeza akasema namuomba Kadinali Pengo naye aje hiyo ni asubuhi sasa tukamtafuta Pengo alikuwa kwenye ibada hakupokea, akaniuliza CDF haujampata Pengo? nikamwambia yuko kwenye ibada baba atakapotoka atakuja, kwahiyo wakaja wote Kadinali Pengo na Father Makubi sasa katika taratibu za kikatoliki wanamsalia ibada na kumpa sakramenti ya upako wa magonjwa aliyekuwa katika hatari ya kufariki”

“Walipomaliza kumsalia akapumzika lakini ilipofika saa nane mchana wakatupigia watu wa hospitali wakanipigia mimi kama Mkuu wa Majeshi, wakampigia DGS na IGP wakatuambia hali ya mheshimiwa siyo nzuri sana hebu njooni, tukaenda tukamkuta ametulia lakini alikuwa hawezi kuongea tena, tukawaita madaktari wengine, nakumbuka tulimuita Profesa Maseru, Profesa Janabi alikuwepo muda wote kwa hiyo yule aliongezea nguvu wakajaribu kumuangalia, tukaendelea kukaa mpaka jioni, ikafika jioni saa kumi na mbili na nusu hivi au saa moja kasoro akakata roho, tukiwepo wakuu wa ulinzi wa vyombo watatu mimi (CDF), IGP na DGS”-Mkuu wa Majeshi mstaafu, Venance Mabeyo.

See also  Jinsi Unyago na Jado zinavyosaidia Kukuza na Kuendeleza Maadili

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

WIMBO MPYA WA ZUCHU "SIJI"
Read more
Leicester coach Cheika banned for disrespecting doctor...
LONDON, - Leicester Tigers head coach Michael Cheika has been...
Read more
WANAFUNZI WAISHITAKI SERIKALI ...
HABARI KUU Wanafunzi wa Korea Kusini wamefungua kesi dhidi ya...
Read more
Anti-discrimination charity Kick It Out says it...
Across all levels of English football last season, there were...
Read more
Hersi Said anavyotembea kwenye kivuli cha Moise...
Rais wa mabingwa wa nchi Young Africans Sports Club Eng...
Read more

Leave a Reply