HABARI KUU
Niger jana imetangaza kuvunja makubaliano ya ushirikiano wa Kijeshi na Merikani, makubaliano yaliyotiwa saini mwaka wa 2012 ikiyaita yasiyokuwa na malengo kwa Niger.
Marekani ina karibu wanajeshi elfu moja nchini humo, pamoja na kituo kikubwa cha Ndege zisizo na rubani huko Agadez.
Katika televisheni ya taifa, Msemaji wa Serikali alituhumu ushirikiano huo usio wa haki na kutokidhi malengo kwa serikali.
Kwa mjibu wa Kanali Meja Amadou Abdramane amesema kuwa makubaliano ya ushirikiano yamekuwa kama maneno tu na kuwafaidisha Wamarekani badala ya Niger huku pia Niamey ikilalamika kutokuwa na taarifa juu ya operesheni za Marekani ndani ya nchi hiyo.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.