NYOTA WETU
Msanii wa Afrobeats kutoka Nigeria Wizkid amewashangaza wengi baada ya kutoa maneno ambayo yamewashtua wadau wengi wa muziki wa Afrika kufuatia kutoa kauli rasmi kuwa yeye sio msanii wa Afrobeats na asihusishwe na chochote kinachohusiana na aina ya muziki huo, Licha ya kuwa muziki huo ndio uliomtambulisha kwenye soko la kimataifa.
Mkali huyo wa muziki Afrika
ametoa kauli hiyo jana kwenye mfululizo wa Insta stories ambapo alikuwa akitangaza ujio wa Album yake mpya ya [Morayo] ambayo itakuwa sio ya muziki wa Afrobeats .
” Album haitakuwa album ya mahadhi ya Afrobeats kwa sababu kadhaa’ kwanini sitaki tena kuitwa msanii wa Afrobeats? Kwa sababu nafanya aina zote za muziki, muziki mzuri lakin sitotaki uwekwe nembo kuwa ni Afrobeats” alisema kupitia insta story.