MICHEZO
Meneja wa Habari na Mawasiliani Yanga SC, Ally Kamwe amesema kuwa kipigo kutoka kwa Azam FC cha mabao 2-1 kimewaongezea hamasa katika mchezo wao war obo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika.
Yanga itacheza dhidi ya Mamelodi Machi 29, mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kisha marudiano kuchezwa April 5 nchini Afrika Kusini.
Yanga ilipoteza mchezo wa pili Ligi Kuu Bara msimu huu ambapo jana ilipoteza katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mabao ya Gibril Sillah na Feisal Salum huku Clement Mzize akifunga kwa upande wa Wananchi.
Aidha,kiungo mshambuliaji Azam FC, Feisal Salum maarufu ‘Fei Toto’ amekiri kuwa licha ya kuifunga timu yake ya zamani ya Yanga jana Machi 17, 2024 lakini mchezo huo ulikuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wao.
Fei Toto mpaka sasa ametupia mabao 13 msimu huu wa Ligi Kuu Bara sawa na mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz KI.