MICHEZO
Serikali kupitia Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, leo Machi 19, 2024 imesaini mkataba wa ujenzi wa uwanja wa michezo utakaopewa jina La Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Uwanja huo utakaojengwa jijini Arusha utagharimu shilingi bilion 286 na unatazamiwa kutumika kwenye michuano ya AFCON 2027 ambapo Tanzania ni moja ya nchi mwenyeji wa mashindano hayo. Nchi nyingine zitakazoshirikiana na Tanzania ni Kenya na Uganda.
Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Damasi Ndumbaro amesema lengo la kujenga uwanja huo jijini Arusha ni kukuza michezo sambamba na sekta ya utalii nchini.
MWONEKANO WA UWANJA WA DKT SAMIA