SERIKALI YAAGIZA MAMLAKA ZOTE KUHUSU UVUNAJI MAJI

0:00

HABARI KUU

Serikali imeziagiza Mamlaka za Maji kushirikiana na Halmashauri zote za Wilaya, kuhamasisha uvunaji wa Maji ya Mvua katika ngazi zote, hasa katika kipindi hiki ambapo zinaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mwajuma Waziri kwa niaba ya Waziri wa Maji, Juma Aweso ameyasema hayo Jijini Dodoma katika uzinduzi wa taarifa ya utendaji wa mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira kwa kipindi cha Mwaka 2022/23.

Amesema, baadhi ya maeneo mvua hizo zimeleta madhara makubwa, hivyo basi, endapo uvunaji wa maji yatapunguza athari na kutaiwezesha nchi na wananchi kuwa na akiba ya maji ambayo yatatusaidia kipindi cha ukame.

Mwajuma ameongeza kuwa, lengo la Maendeleo Endelevu (SDGs) ya mwaka 2030 hususan namba 6 linaeleza umuhimu wa Majisafi na Usafi wa Mazingira.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji(EWURA), Dkt. James Andilile amesema Pamoja na kuimarika kwa utendaji kazi wa mamlaka za maji katika kutoa huduma,uchambuzi umebainisha changamoto zinazozikabili mamlaka za maji ni pamoja na Kutokidhi kiwango cha dawa (residual chlorine levels) katika maji yanayosambazwa Majitaka yaliyotibiwa kutokidhi viwango vya ubora kwenye viashiria vya mahitaji ya oksijeni kibiolojia na kikemikali (BOD na COD).

Amesema, “changamoto nyingine ni Uwiano mdogo wa idadi ya watu wanaopata huduma ya majisafi na usafi wa mazingira,Upotevu mkubwa wa maji wa zaidi ya asilimia 20 inayokubalika,Uchache wa miundombinu ya miundombinu ya kutibu majitaka na topetaka kinyesi,Uwiano mdogo wa uzalishaji wa maji ikilinganishwa na mahitaji,Bei za maji za muda mrefu ambazo haziendani na gharama halisi za uendeshaji naUpatikani wa huduma isiyotesheleza ya usafi wa mazingira.”

“Na kwa ujumla, utendaji wa mamlaka za maji na usafi wa mazingira umeendelea kuimarika Kwa mwaka 2022/23, Mamlaka za Maji 78 kati ya 85 zilipata alama kuanzia wastani hadi vizuri sana katika utendaji wa ujumla ikilinganishwa na mamlaka 77 kati ya 90 kwa mwaka 2021/22,” amesema Andilile

See also  Nyumba za Mfanyabiashara na Mwanamuziki Sean ‘Diddy’ Combs zilizopo Los Angeles na Miami zimevamiwa na Maafisa Usalama ikidaiwa wanafanya uchunguzi na upekuzi kuhusu tuhuma za Biashara ya Ngono na Biashara ya Binadamu zinazotajwa kuhusu staa huyoMaafisa wa HSI ambacho ni Chombo Kikuu cha Uchunguzi cha Idara ya Usalama wa Taifa ya Marekani wamewafunga pingu baadhi ya Watu waliokutwa katika nyumba ya Los Angeles wakiwemo Watoto wa Diddy ambao ni King na Justin huku baba yao akiwa hajulikani alipo.Inadaiwa ndege Binafsi ya Diddy imeonekana ikielekea Visiwa vya Caribbean kwa mujibu wa Tovuti ya Flight Tracking Data.
Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Great Blue Heron working on its catch
Ac tortor dignissim convallis aenean et tortor at. Nisl...
Read more
Banda brace sends pride into play off...
Zambian forward Barbra Banda scored a brace in a player...
Read more
SUNNA SEPETU AKUMBWA NA MKASA WA UTAKATISHAJI...
HABARI KUU Dada wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Sunna...
Read more
KANYE WEST NA WAYAHUDI MAMBO NI SAFI
NYOTA WETU. Mwanamziki na mfanyabiashara wa Marekani, Kanye West ametoka hadharani...
Read more
SPIKA WA BUNGE ANASURIKA KULALA JELA ...
HABARI KUU Aliyekuwa Spika wa Bunge la Afrika Kusini Nosiviwe...
Read more

Leave a Reply