DONALD TRUMP AOMBA URAIS ILI KUMFUKUZA PRINCE HARRY

0:00

HABARI KUU

Mgombea urais Donald Trump amesema kama atashinda urais Novemba mwaka huu atamfukuza mwana mfalme wa Uingereza, Prince Harry iwapo atakuwa amedanganya kuhusu utumiaji wake wa dawa za kulevya kwenye fomu ya kuomba viza ya kuishi Marekani.

Trump (77) ambaye juzi kwenye jimbo la Ohio alionyesha kukerwa na wingi wa wahamiaji na kuwaita wanyama na wahalifu waliohamia Marekani, ametoa kauli ya kumfukuza Prince Harry kwenye mahojiano maalumu aliyofanya jana Jumatatu na mtangazaji Nigel Farage wa televisheni ya GB News.

Kwenye mkutano wake wa hadhara huko Ohio, Trump amemtuhumu Rais Joe Biden kwa kuruhusu uingiaji wa wahamiaji haramu, akisema wameleta uhalifu Marekani aliouita ‘uhalifu wa kuhamia wa Biden.’

Prince Harry ni mtoto wa Mfalme Charles III wa Uingereza, lakini anaishi Marekani alikohamia mwaka 2020 akiwa na familia yake akiwamo mkewe Meghan Markle na watoto wao Archie na Lilibet.

Mama yake Harry, Princess Diana alifariki dunia kwa ajali ya gari nchini Ufaransa Agosti 31, 1997 na kuwaacha na kaka yake William wakiwa bado wadogo. Trump kwenye mahojiano hayo amesema akichaguliwa kuwa Rais wa Marekani, Prince Harry hatopata upendeleo maalumu iwapo alidanganya kwenye maombi yake ya viza kuhusu rekodi yake ya matumizi ya dawa za kulevya kama cocaine, bangi na mchanganyiko wa uyoga.

Prince Harry kwenye kitabu cha kumbukumbu ya maisha yake ameelezea kifo cha mama yake Princess Diana, mgogoro na kaka yake William na pia amekiri kutumia dawa za kulevya.

Amesema ametumia cocaine mara nyingi wakati huo akiwa na umri wa miaka 17 ili imsaidie kujihisi tofauti, amevuta bangi na matumizi ya uyoga uliotengenezwa kama kilevi.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

See also  Pieter-Steph du Toit and Ellie Kildunne named world rugby’s best players

Related Posts 📫

WATOTO WATATU WAFARIKI KWA KUANGUKIWA NA NYUMBA...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
Valencia striker Rafa Mir has been released...
Mir, 27, appeared in court in Valencia on Wednesday after...
Read more
Moment Davido composure crumbles as Chioma unleashes...
Witness the electrifying moment captured in these captivating videos. Davido and...
Read more
MWIMBAJI AFARIKI AKIWA ANATUMBUIZA ...
HABARI KUU Muimbaji wa Injili nchini Brazil, Pedro Henrique(30)...
Read more
KANUNI 14 ZINAZOWEZA KUKUONGOZA KWENYE MAHUSIANO ...
MAPENZI. Mwongozo ni kama katiba ilivyo ambako kanuni na sheria...
Read more

Leave a Reply