NYOTA WETU
Polisi nchini Marekani wanaendelea na uchunguzi juu ya kifo cha mpenzi wa Nyota wa Tennis Aryna Sabalenka kinachosadikiwa kuwa ni cha kujiua.
Konstantin Koltsov (42) wa Belarus ambaye ni mchezaji wa kulipwa wa Ice Hockey alikutwa akiwa amefariki ndani ya Hoteli huko Miami, Florida.
Kifo cha Mwanamichezo huyo kilitangazwa na klabu ya Salatav Yulaev ya Urusi ambapo Koltsov aliwahi kuichezea na baadaye kuwa kocha msaidizi.
Mwaka 2002 na 2010 aliichezea timu ya taifa ya Belarus katika michuano ya Winter Olympics.
Bi.Sabalenka ambaye ndio mpenzi wa marehemu yupo Miami na anatarajia kucheza mechi yake ya kwanza katika michuano ya Miami Open Ijumaa ijayo.
Taarifa zinaeleza kuwa Bi.Sabalenka ambaye kwa sasa anashikilia nafasi ya 2 duniani kwa ubingwa upande wa wanawake, anatarajia kucheza mechi yake kama ilivyopangwa.