SABABU MAKAMU WA RAIS KUMWAKILISHA RAIS SAMIA KWENYE KIKAO CHA DHARURA SADC

0:00

HABARI KUU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Utatu wa Asasi mbili za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika Lusaka, Zambia Machi 23, 2024.

Makamu wa Rais ataondoka nchini Machi 22, 2024 kushiriki Mkutano huo ambao agenda kubwa ni hali ya ulinzi na usalama katika nchi za SADC, hususan katika Jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji na Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Mkutano huo utatanguliwa na Mikutano ya maandalizi ya ngazi za Wataalam ambayo ilianza tarehe 17 Machi 2024 na itakamilishwa na Mikutano ya Makatibu Wakuu na Mawaziri itakayofanyika Machi 22, 2024.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba ataungana na Mawaziri wenzake kutoka nchi wanachama katika Mkutano huo muhimu.

Tanzania kama mwanachama wa SADC na ikiwa ni miongoni mwa nchi zinazochangia vikosi vya kulinda amani katika nchi za Msumbiji na DRC inashiriki kikamilifu katika ngazi zote za Mkutano huo.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

USALITI WA NEYMAR KWENYE NDOA WABAINIKA
NYOTA WETU. Neymar Jr na mpenzi wake,Bruna Biancardi wametengana...
Read more
BOBRISKY FAILS TO MEET BAIL CONDITIONS ...
OUR STAR 🌟 Popular crossdresser Bobrisky has reportedly failed to...
Read more
2027: Atiku, Obi, Kwankwaso Working on possible...
The Deputy National Spokesman of the Peoples Democratic Party (PDP),...
Read more
SABABU WAZIRI WA MAJI JUMAA AWESO KWENDA...
HABARI KUU
See also  AUWA MKE WAKE KISA MALI
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Hamidu Aweso (Mb),...
Read more
Stuttering Arsenal need big statement against Liverpool
Arsenal's serene start to the season has hit stormy waters...
Read more

Leave a Reply