SABABU WAZIRI MKUU WA IRELAND LEO VARADKAR KUJIUZULU

NYOTA WETU

Waziri Mkuu wa Ireland Leo Varadkar ametangaza kujiuzulu.

Varadkar (45) alikiongoza Chama cha Fine Gael tangu mwaka 2017 na kushika nafasi ya Uwaziri Mkuu mara mbili.

Akitoa tangazo hilo kwa hisia kubwa, Bw.Varadkar amesema sababu zake za kujiuzulu ni za binafsi na za kisiasa.

“Baada ya miaka 7 kwenye ofisi, sidhani kama mimi ni mtu bora zaidi kwa kazi hii”

“Naamini Kiongozi mpya atakuwa na nafasi nzuri zaidi yangu, kupata viti kwa ajili ya Chama cha Fine Gael katika uchaguzi mkuu ujao”

“Wanasiasa nao ni binadamu na tuna mapungufu, tunajitahidi lakini inafika hatua hatuwezi tena, hivyo tunaacha na kusonga mbele”.

Varakdar alikuwa mtu mwenye umri mdogo kuliko wote kuwahi kushika nafasi ya Uwaziri Mkuu nchini Ireland akiwa na umri wa miaka 38.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related News 📫

Uwanja wa Uhuru kukarabatiwa kwa bilioni 19
MICHEZO Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara...
Read more
Rulani: Sundowns sacking me doesn't make sense,...
Having won the DStv Premiership for the third time in...
Read more
8 REASONS WHY MEN BREAK UP WITH...
The end of a relationship can feel like the end...
Read more
See also  Utata ajali ya Raisi wa Iran

Leave a Reply