HABARI KUU
Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni ameomba kulipwa fidia ya euro 100,000 kutokana na video chafu za bandia zilizotengenezwa kumuhusu na kuwekwa mtandaoni.
Picha bandia ni ile ambayo uso wa mtu huungwa na mwili wa mtu mwingine kidigitali.
Bi.Meloni anatarajia kutoa ushahidi Mahakamani katika mji wa Sardinia ifikapo Julai 2.
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 40 pamoja na baba yake mwenye umri wa miaka 73 wanatuhumiwa kutengeneza video hizo chafu.
Picha hizo zilipostiwa kwenye mtandao mmoja wa nchini Marekani unaohusika na picha chafu ambamo video hizo zilitizamwa na mamilioni ya watu ndani ya miezi kadhaa.
Polisi nchini Italia wamesema wamefanikiwa kuwapata watuhumiwa kwa kuifuatilia simu waliyoitumia kuposti video hizo mtandaoni.
Wawili hao wanashtakiwa kwa kosa la kumkashifu na kumchafua Bi.Meloni, ambapo chini ya sheria za Italia kosa hilo linaweza kuwa la jinai na linaweza kupelekea hukumu ya kifungo cha jela.