NYOTA WETU
Mwaka wa 2002, Muhammad Ali alipewa nyota ya heshima kwenye ‘Hollywood Walk of Fame’ lakini haikuwa kama nyota zingine.
Kinyume na desturi, nyota yake ilikuwa imewekwa kwenye ukuta badala ya kwenye lami,kwenye eneo la burudani la ‘Kodak Theater’.
Kwa sababu bingwa huyo wa zamani, aliyekuwa na miaka 59 wakati huo, alisema hakutaka jina lake liwekwe chini na watu walikanyage maana jina lake limefanana na kiongozi mkubwa wa dini ya uislamu.
“Nimechukua jina la Mtume wetu mpendwa Mohammed (S.A.W), na haiwezekani niache watu walikanyage jina lake,” alisema.
Nyota ya Ali ndiyo pekee ambayo jina lake halipo sakafuni, badala yake imewekwa ukutani.
Nyota yake ilitolewa baada ya kamati kuamua kuwa ngumi inaweza kuchukuliwa kama aina ya mchezo wenye mchango kwa tasnia ya burudani.
Bingwa huyo wa zamani wa ngumi alifariki akiwa na umri wa miaka 74 baada ya kupelekwa hospitalini kwa matatizo ya kupumua. Alikuwa akikabiliana na ugonjwa wa Parkinson kwa zaidi ya miaka 30.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.