MAHAKAMA YAJIFUNGA KWA KAULI YA JAJI MKUU

0:00

HABARI KUU

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amesema wataendelea kusimamia na kuhakikisha sheria zinatumika vyema katika utoaji wa haki kwa wananchi na kuyafikia malengo yaliyotajwa katika dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.

Prof. Ibrahim ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mkuu wa Chama cha Mawakili wa serikali Tanzania, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Amesema, “kazi zetu zinaongozwa na malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, hivyo tufanye kazi kwa kuzingatia hayo ikiwemo kujenga amani, mshikamano, kuboresha Maisha ya Mtanzania kwa kuelekeza nguvu ya sheria katika kuboresha Maisha yao na kuimarisha Utawala bora.”

Serikali imetekeleza mpango wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama Jijini Dodoma, Vituo sita Jumuishi vya Utoaji Haki, Mahakama za Wilaya 27 pamoja na mahakama za mwanzo 14 huku ikiendelea na ujenzi wa vituo jumuishi sita vya Geita, Simiyu, Njombe, Katavi, Songea na Songwe.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Southampton must sack Russell Martin immediately
Don't miss out!
Invalid email address