MICHEZO
Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City huenda ikamuachia winga wao Jack Grealish, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa ajli ya kupata pesa itakazozitumia kufanya usajili wa mastaa mbalimbali inaowahitaji katika dirisha lijalo.
Grealish amekuwa hapati nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza cha Man City. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.
Staa huyo mwenye umri wa miaka 28 hajaonyesha kiwango kilichotarajiwa tangu kuanza kwa msimu huu na kocha wa Man City Pep Guardiola, alishawahi kutamka wazi kwamba haridhishwi na kiwango chake.
Kuna ripoti zinazoeleza kuwa Man City inataka kumsajili winga wa SSC Napoli Khvicha Kvaratskhelia katika dirisha lijalo, ili akachukuwe nafasi ya Grealish.
Tangu dirisha lililopita kumekuwa na taarifa zinazomhusisha Grealish na Arsenal inayodaiwa kuandaa zaidi ya Pauni 50 milioni kwa ajili ya kufanikisha mchakato wa kumsajili.
Pep anawania taji la Ligi Kuu England analolishikilia na amekuwa akitumia wachezaji wanaompa matokeo, kwani vita ya ubingwa ni kali mbele ya Arsenal na Liverpool. Grealish amekuwa akianzia benchi au kutokucheza na hii inachangia kutaka kuondoka.