MASTORI
Siku mbili baada ya watoto waliokuwa na uzito kupita kiasi, Imani na Gloria Joseph kuruhusiwa kutoka hospitalini, kilichobainika chatajwa, huku Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ikiingia katika hatua ya pili ya uchunguzi.
Hayo yamesemwa jana Alhamisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi wakati wa mahojiano na vyombo vya habari.
Amesema baada ya kuwapima vipimo mbalimbali vya mafuta, moyo, figo, kisukari na vipimo vingine vikubwa kama CT Scan, MRI na vinginevyo watoto hao hawajabainika kuwa na tatizo lolote laa kiafya.
“Tunakwenda hatua ya pili kwa sababu hawa wote wanapimwa kupitia gharama za Serikali hakuna wanacholipa….mwisho lazima kujua ni jeni gani ambayo imeleta hitilafu kubwa namna hii kwa mtoto wa miaka mitano kuwa na uzito wa kilo 61. Ni tatizo ambalo tunalifanyia uchunguzi, tukiweza kugundua kwanza itatusaidia kuelimisha hospitali na taasisi nyingine, wazazi, ndugu na jamiii kwa ujumla,” amesema Profesa Janabi.