NYOTA WETU
Ripoti zinasema kuwa mchezaji kandanda wa zamani Robinho alikamatwa huko Santos, Brazil, baada ya Mahakama ya juu kukataa ombi lake la kuachiliwa Alhamisi ili kutumikia kifungo chake cha miaka tisa jela ambapo alihukumiwa nchini Italia kwa ubakaji.
Mawakili wa Robinho walikuwa wamekata rufaa katika Mahakama ya juu ya shirikisho (STF) siku ya Jumatano kwa matumaini kwamba ingesitisha agizo la kufungwa jela.
Polisi wamefahamisha kwamba Robson de Souza, alikamatwa katika mji wa Santos, anakoishi na Robinho, 40 atahamishiwa kwenye Gereza la Tremembé, kilomita 150 kutoka Sao Paulo.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City aliyecheza mechi 100 akiwa na klabu hiyo alikutwa na hatia ya kumbaka msichana wa Kialbania ambaye alikuwa akisherehekea miaka 23 katika klabu ya usiku ya Milan.