HABARI KUU
Jeshi la Polisi Kanda Maalum linawashikilia Claudian Makaranga (28) Mkazi wa Kawe, na Raia wa China, Hongliang Yang (35), kwa tuhuma za kuingiza Nchini vifaa vya Mawasiliano ya Intaneti vyenye jina la STARLINK KIT/DEVICE bila kufuata utaratibu wa Kisheria
Watuhumiwa hao wamekuwa wakijitangaza kupitia Mitandao kama Instagram kwa kuuza Vifaa na kutoa huduma ya Intaneti huku baadhi ya vifaa vilivyoingizwa nchini imebainika vilishauzwa na kutumika katika baadhi ya maeneo ya Dar
Februari 26, 2024, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, kupitia Mtandao wa X (Twitter) alisema Kampuni ya Starlink inayotoa Huduma za Intaneti kwa kutumia ‘Satelaiti’ inakamilisha hatua za mwisho ili kupata vibali vya kutoa Huduma Nchini.