HABARI KUU
Bunge la Tanzania limekanusha madai yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe ambapo alidai kwamba mishahara ya Wabunge imeongezwa mwaka 2023 kutoka shilingi milioni kumi na tatu (sh.13,000,000/=) hadi shilingi milioni kumi na nane (sh.18,000,000/=)
Madai hayo aliyetoa jana ijumaa tarehe 22 Machi, 2024 alipokuwa anahutubia mkutano wa hadhara Mjini Babati Mkoa wa Manyara
Taarifa ya Bunge imeeleza kuwa taarifa hizo ni uzushi na kueleza kuwa hakuna mbunge aliyeongezewa mshahara na nyongeza ya mishahara ni suala linalozingatia bajeti
“Tunapenda kuujulisha umma kwamba madai hayo ni uzushi na upotoshaji kwa kuwa hakuna Mbunge aliyeongezewa mshahara kama alivyodai. Hivyo, tunapenda kuwashauri na kuwasihi wananchi kupuuza madal hayo ambayo lengo lake ni kuleta taharuki pamoja na kuwagombanisha wananchi na wawakilishi wao”
“Nyongeza ya mshahara ni suala linalozingatia bajeti na hakuna utaratibu wa aina yoyote kama huo ambao umefanyika kwa ajili ya kuwaongezea Waheshimiwa Wabunge mishahara” imeeleza taarifa hiyo ya bunge .