0:00
MICHEZO
Malaysia imekuwa nchi ya pili kulikataa jukumu la uenyeji wa michezo ya Jumuiya ya Madola kwa mwaka 2026.
Hali hii inayaweka mashindano hayo kwenye wasiwasi wa kufutwa kwa mara ya kwanza tangu vita kuu ya Pili ya Dunia.
Nchi hiyo ambayo ilikuwa mwenyeji wa michezo hiyo mwaka 1998 ilikubali kuchukua jukumu baada ya jimbo la Victoria, nchini Australia kuamua kujitoa Julai 2023 kwa sababu za kifedha.
Maafisa nchini humo wamesema Shirikisho la michezo ya Umoja wa Madola(CGF) limetoa fungu la pauni milioni 100 kiasi ambacho hakitoshi.
Naye Msemaji wa Serikali ya Malaysia Fahmi Fadzil amesema “tungekuwa na muda wa kutosha tungeweza kuandaa, lakini muda ni mfupi hivyo hatutoweza”.
Related Posts 📫
The announcement has elicited numerous reactions from netizens.
Paul Okoye, the...
PROLONGING SILENT TREATMENT WHEN OFFENDED TO SHOW YOU ARE ANGRYThis...
Provide a clean and comfortable living environment for your chickens....
MAGAZETI
Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...