NYOTA WETU
Baada ya Princess Catherine Elizabeth Middleton maarufu kama Princess Kate ambaye ni Mke wa Prince William wa Wales, mrithi wa ufalme wa Uingereza kutoonekana kwa muda mrefu na kuibua maswali na taharuki kwa watu wengi nchini Uingireza huku hofu ikitanda juu ya Afya yake.
Hatimaye Princess Kate leo Ijumaa ameonekana kwenye kipande cha video kilichoonyeshwa kupitia ukurasa rasmi wa falme ya Uingereza akisema kuwa yupo salama na alikuwa akipatiwa matibabu ya kemikali baada ya upasuaji kubaini kuwa ana saratani.
Kupitia video hiyo amewashukuru watu wote waliotuma ujumbe kutaka kujua hali yake na kuonesha kujali kwa kutoonekana na kuomba apewe faragha na familia yake Wakati huu anapoendelea kupatiwa matibabu.
Hata hivyo mpaka Sasa Binti huyo wa mfalme hajaweka wazi anaumwa aina gani ya saratani.
Princess Catherine Elizabeth Middleton aliolewa na Prince William, “The Prince of Wales”, huko Westminster Abbey tarehe 29 Aprili 2011.
Wawili hao wamefanikiwa kupata watoto watatu ambao ni Prince George, Princess Charlotte na Prince Louis.