HABARI KUU
Related Content
Related Content
Raia wa Senegal leo March 24,2024 wanapiga kura kumchagua Rais wa Nchi hiyo.
Kura za Uchaguzi Mkuu utakaoamua muelekeo mpya wa Taifa hilo zinatarajiwa kupigwa leo ambapo Wagombea 19 wanawania nafasi ya Urais kwa lengo la kumrithi Rais Macky Sall atakayemaliza utawala wa miaka 12 ifikapo Aprili 2, 2024
Taarifa kutoka Senegal zinaeleza kuwa licha ya wingi wa Wagombea, wanaotajwa kuwa na nafasi zaidi ya kushinda ni Bassirou Diomaye Faye anayeungwa mkono na Wafuasi wa Ousmane Sonko kutoka upande wa Upinzani na Amadou Ba anayeungwa mkono na Chama Tawala
Ili Mgombea atangazwe mshindi na kuepuka marudio ya uchaguzi, atalazimika kupata 50% ya Kura.
