BILA NGUMI TANZANIA INGETOKA PATUPU MASHINDANO YA AFRIKA GHANA

0:00

MICHEZO



Kikosi cha Timu ya Taifa ya Ngumi ya Tanzania maarufu kama “Faru Weusi wa Ngorongoro” wamefanikiwa kuiheshimisha Tanzania katika michezo ya 13 ya Afrika (All African Games 2023) Jijini Accra nchini Ghana inayofungwa rasmi usiku wa leo katika Jiji hilo.

Kikosi hicho kimefanikiwa kushinda Medali 3 za shaba katika mashindano hayo kutoka kwa wachezaji Light Heavyweight Yusuf Changalawe (Nahodha), Lightweight Ezra Paulo Mwanjwango na Cruiserweight Musa Maregesi.

Wachezaji wote hao wanatokea katika Klabu ya Ngome inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)

Katika sherehe za utoaji wa medali kwa washindi katika mchezo wa ngumi, iliyofanyika usiku wa Machi 23, 2024 katika ukumbi wa Bukom Arena, Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirikisho la Ngumi Bara la Afrika (AFBC) alikuwa kuwa mgeni rasmi katika kuwavalisha washindi wa Uzani wa Ligh Heavyweight 80kg kwa Wanaume na Cruiserweight 86kg, ambapo Changalawe na Maregesi walikuwa moja ya washindi katika uzani hizo.

Kikosi hicho cha Faru Weusi wa Ngorongoro pamoja na wachezaji wa michezo mingine walioiwakilisha Timu Tanzania katika michezo hiyo, wanatarajia kurejea Dar es salaam Machi 25, 2024 saa 9.40 usiku.

Aisha, kikosi hicho kikirejea kitaendelea na mazoezi ya kujiandaa kushiriki mashindano ya Mandela “Mandela Cup” yatakayofanyika Durban, Afrika ya Kusini kuanzia tarehe 15-23 April, 2024.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Justin Bieber and his wife Hailey Bieber...
Beloved Canadian pop sensation Justin Bieber and his wife Hailey...
Read more
President Bola Tinubu is set to transmit...
According to Minister of Information and National Orientation, Mohammed Idris,...
Read more
Real's Vinicius out of Champions League clash...
MADRID, - Real Madrid forward Vinicius Jr will miss his...
Read more
Injuries cost top league 732 million euros...
Players in Germany's Bundesliga are most likely to be injured...
Read more
KIONGOZI MKUU WA AL-SHABAAB AUAWA
HABARI KUU
See also  JE TIMU YA CHELSEA INAENDA KUTAWALA SOKA ?
Kiongozi mkuu wa kundi AL-SHABAAB linaloendesha harakati...
Read more

Leave a Reply