NYOTA WETU
Kiungo Christoph Baumgartner wa Austria jana alifunga bao ndani ya sekunde 6 za mechi na kuvunja rekodi ya bao lililofungwa kwa haraka zaidi katika soka la Kimataifa.
Baumgartner (24) anayeichezea RB Leipzig ya Ujerumani pamoja na timu ya taifa ya Austria aliifunga bao hilo wakati wa mechi ya kirafiki kati ya Austria na Slovakia Mjini Bratislava.
Juhudi za kiungo huyo zilikuwa za haraka hadi kumshinda Lukas Podolski aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo baada ya kuifungia Ujerumani bao katika sekunde ya 7 wakati wa mechi dhidi ya Ecuador mwaka 2013.
Hata hivyo mtandao unaohusika na rekodi za dunia wa ”Guiness World Records” bado haujaweza kuthibitisha kama bao hilo ndio bao rasmi lililofungwa kwa haraka zaidi kupitia kick-off kwa kuwa mtandao huo haufiatili mabao nje ya soka la kulipwa.