MASTORI
Related Content
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amesema Dunia tuliyopo sasa ingekuwa na nusu ya Viongozi Wanawake basi ingekua bora zaidi ya ilivyo hivi sasa.
Prof. Mkumbo ameyasema hayo kwenye kilele cha utoaji wa tuzo za Malkia wa Nguvu 2024 zilizoandaliwa na Clouds media Group kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam, na kusema ni lazima kumuinua Mwanamke kama tunataka Dunia iwe bora zaidi.
Malkia wa Nguvu ni tuzo zinazotolewa kila mwaka kwa mwaka wa nane mfululizo ambapo kwa mwaka huu 2024 aina 9 zimetolewa kutoka kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu, Ubunifu na Huduma za Jamii.
