NYOTA WETU
Ndoa ya Nyota wa zamani wa Chelsea na timu ya Taifa ya Cameroon, Geremi Njitap ipo katika mchakato wa talaka baada ya kubainika Watoto Mapacha waliozaliwa Mwaka 2008 miaka minne kabla ya kufunga ndoa na mkewe, Toukam Fotso Laure Verline si wake Kibaiolojia
Geremi (45) amefungua kesi Mahakamani akitaka ndoa ivunjike baada ya Vipimo vya Vinasaba (DNA) kuonesha Mapacha hao ambao mkewe alimuaminisha ni wa kwake, ni wa mwenza wa zamani wa Toukam.
Nyaraka zilizovuja Mtandaoni zimeonesha Geremi amelalamika kukosewa heshima na mkewe ambaye alikuwa akimtolea lugha ya dharau mbele ya Watoto hao pia walikuwa na migogoro ya mara kwa mara.
Geremi akiwa Beki wa Kulia mwenye uwezo wa kucheza nafasi ya Kiiungo Mkabaji alicheza pia katika Timu za Chelsea ,Real Madrid, Middlesbrough na Newcastle United.