SERIKALI YA NIGERIA YAFANIKIWA KUWARUDISHA MATEKA 137

0:00

HABARI KUU

Maafisa nchini Nigeria wamethibitisha kuokolewa kwa watu 137 waliotekwa na watu wenye silaha huko Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo wiki mbili zilizopita.

Taarifa zimeeleza kuwa operesheni ya uokoaji ilifanyika alfajiri ya leo ikiwa ni siku chache kabla ya tarehe ya mwisho ya malipo yaliyoombwa na watekaji hao.

Gavana wa Jimbo la Kaduna Uba Sani amesema wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa shule wameokolewa kutokana na ujasiri wa maafisa wa usalama.

Wiki iliyopita majambazi hao walidai kiasi cha pauni 486,000 ili kuwaachia watu hao, hata hivyo Rais Bola Tinubu aliahidi kuwaokoa bila ya kulipa hata senti moja.

Idadi ya wanafunzi na wafanyakazi wa shule waliotekwa katika wiki za hivi karibuni ni 287 hivyo takribani nusu yao bado wanashikiliwa mateka.

Majambazi hao wamekuwa wakiwateka nyara maelfu ya watu katika miaka ya hivi karibuni nchini humo na kuwaachia huru mara baada ya kulipwa.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

JONAS MKUDE AMSHTAKI MO DEWJI ...
NYOTA WETU Mchezaji wa klabu ya Yanga, Jonas Mkude amefungua kesi...
Read more
Pogacar caps incredible season with fourth successive...
World champion Tadej Pogacar rounded off his remarkable season by...
Read more
TAARIFA ZA UONGO WALIZO NAZO WANAWAKE KUHUSU...
MAPENZI 1. WANAUME WOTE NI SAWA. Kaka au ndugu yako...
Read more
Minimum Wage: Be Patient With Tinubu, Presidency...
The Presidency on Monday appealed to Nigerians not to pile...
Read more
"WHY ARE MEN JUMPING ON THE 'ESTHER...
OUR STAR 🌟 "Why are men jumping on the 'Esther'...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  RAIS YOWERI MUSEVENI AMTEUA MWANAE KAINERUGABA KUWA MKUU WA MAJESHI

Leave a Reply