MICHEZO
Siku chache baada ya Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo , Mh. Damas Ndumbaro kutoa kauli iliyoonekana kuchanganya watu kuelekea katika Michezo ya kimataifa inayozihusu Simba sc tanzania na yanga sc , Serikali imetokeza na kutoa neno juu ya kauli ya Waziri Ndumbaro.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema
“Lugha za michezo, utani ni kitu cha kawaida, mnapozungumza 80% ni utani na 20 ndio ukweli, mkizungumza habari za Simba SC na Yanga SC ukang’ang’ana kitu kama kilivyoandikwa utafika hatua utawachosha watu.”
Matinyi amesema hayo wakati akitoa ufafanuzi juu ya hoja ya Waziri Ndumbaro aliyedai ukaguzi utafanyika Uwanja wa Mkapa kwa mashabiki watakaovaa jezi za timu za wapinzani wakati wa michezo ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo Yanga SC na Simba SC ni washiriki.
Amesema “Si kweli kuwa Waziri alimaanisha kutakuwa na ukaguzi wa Passport, anayehusika na ukaguzi ni Idara ya Uhamiaji ambayo hakuitaja alipozungumza, watu wamekomaa na utani hadi Mamelodi Sundowns wamesikia, wameingia uoga hadi TFF wameamua kuandika barua kuwaeleza suala hilo halipo.”