BASSIROU DIOMAYE FAYE MBIONI KUWA RAIS MPYA WA SENEGAL

0

0:00

NYOTA WETU

Kiongozi wa upinzani Bassirou Diomaye Faye ameibuka kuwa anayepewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi wa urais nchini Senegal, baada ya wapinzani kadhaa kukubali kushindwa.

Mamilioni ya watu walishiriki katika upigaji kura siku ya Jumapili, kufuatia miaka mitatu ya misukosuko na maandamano ya upinzani dhidi ya Rais aliyemaliza muda wake, Macky Sall.

Wapiga kura walikuwa na chaguo la wagombea 19, Hata hivyo chaguo la muungano unaotawala, Amadou Ba, alikanusha ripoti za kushindwa na kusema kuwa anatazamia kushiriki katika duru ya pili ya kura ili kuamua mshindi.

Bw Faye, 44, mwanachama wa chama cha Pastef kinachoongozwa na Ousmane Sonko, ambaye alikuwa gerezani siku chache kabla ya uchaguzi na kuondolewa kwenye kinyang’anyiro hicho kwa sababu ya kukutwa na hatia ya kumharibia jina.

Matokeo ya awali yaliyotangazwa kwenye televisheni yalionyesha Bw Faye amepata kura nyingi, na hivyo kusababisha sherehe kubwa mitaani katika mji mkuu wa Dakar na kupelekea wafuasi kuanza kurusha fataki na kupeperusha bendera za Senegal na kupuliza mavuvuzela kwa furaha.

Matokeo hayo pia yalipelekea wagombea watano wa upinzani kumtangaza Bw Faye kuwa mshindi. Anta Babacar Ngom, mmoja wa waliotangulia, alimtakia mafanikio Bw Faye katika taarifa yake.

Bw Sonko alimuunga mkono Bw Faye, mwanzilishi mwenza wa chama chake kilichofutwa cha Pastef, ambaye pia alizuiliwa takriban mwaka mmoja uliopita kwa mashtaka yakiwemo ya kukashifu na kudharau mahakama.

Sheria ya msamaha iliyopitishwa mwezi huu iliruhusu kuachiliwa kwao kabla ya siku ya kupiga kura.

Wamefanya kampeni pamoja chini ya bango “Diomaye ni Sonko”. Baadhi ya wanasiasa mashuhuri na wagombeaji wa upinzani wameunga mkono kugombea kwa Bw Faye.

See also  ODM Party Backs Raila's Call for Dialogue Amid Protests Against Ruto
Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading